• Malalamiko
    • Wasiliana Nasi
    • MMM
    • Barua pepe za Watumishi
Local Government Loans Board

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Makatibu Waliowahi Kuongoza Bodi
    • Orodha ya Wajumbe wa Bodi
    • Orodha ya Mawaziri TAMISEMI
  • Huduma
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo
  • Machapisho
    • Taarifa
    • Kanuni
    • Kuomba Mkopo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
  • Miradi
    • Miradi iliyokwisha
    • Mwongozo wa Uombaji wa Mkopo

MWENENDO WA UREJESHAJI MIKOPO KWENYE HALMASHAURI UNARIDHISHA - DKT. FESTO DUGANGE.

Posted on: May 8th, 2025

OR - TAMISEMI

Serikali kupitia Ofisi ya Rais – TAMISEMI imesema mwenendo wa urejeshaji wa mikopo yote iliyotolewa kwa vikundi vya wanawake, wajasiliamali, watu wenye ulemavu na vijana kabla ya Aprili 2023 ni wenye kuridhisha na Serikali imeendelea kusimamia ili kuhakikisha pesa yote iliyokopeshwa inarejeshwa.

Hayo yamesemwa leo Mei 08, 2025 bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe. Dkt. Festo Dugange  wakati akijibu swali la msingi la Mheshimiwa Mwantumu Haji Mbunge wa Viti Maalum aliyetaka kujua ni lini Serikali itaanza kuwapatia Mikopo Wajasiriamali Wadogo Wanawake na Vijana. 

Katika majibu yake Naibu Waziri Dkt. Dugange amesema, Serikali ilifanya tathimini juu ya utaratibu wa mwanzo uliokuwa ukitumika kutoa na kurejesha mikopo na ilibaini uwepo wa mianya ya kufanya vikundi kutorejesha mikopo kwa ufanisi na kwa wakati unaotakiwa ndiyo maana serikali ilisitisha mikopo hiyo na kuandaa kamati mpya, utaratibu na kanuni kwa ajili ya kusimamia mikopo hiyo katika maeneo yote ya halamashauri.

“Mheshimiwa Spika, Serikali ilisitisha kwa muda utoaji wa mikopo ya asilimia 10 katika mamlaka za serikali za mitaa Aprili 2023 kwa lengo la kufanya maboresho. Aidha, mikopo hii ilianza kutolewa tena tarehe 01 Julai, 2024 kwa mujibu wa Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa na Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo kwa Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu za mwaka 2024” alisema Naibu Waziri Dkt. Dugange.

Aidha aliongeza kuwa “Mheshimiwa Spika, Katika mwaka wa fedha 2024/25, Serikali kupitia halmashauri ilitoa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 82.84 kwa vikundi 8,275 vya wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu. Kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 40.71 zilitolewa kwa vikundi vya wanawake, shilingi bilioni 36.64 kwa vikundi vya vijana, na shilingi bilioni 5.48 kwa vikundi vya watu wenye ulemavu”.Amefafanua Mhe. Dugange

Matangazo

  • RAIS SAMIA AIWEZESHA REA BILIONI 96.8 UTEKELEZAJI MIRADI YA UMEME VIJIJINI DODOMA May 13, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA KUHUSU WAHITIMU WA KIDATO CHA NNE,2023 KUFANYA MABADILIKO YA TAHASUSI ZA KIDATO CHA TANO NA KOZI ZA VYUO KWA MWAKA 2024 March 20, 2024
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • MWENENDO WA UREJESHAJI MIKOPO KWENYE HALMASHAURI UNARIDHISHA - DKT. FESTO DUGANGE.

    May 08, 2025
  • MAFUNZO YA UANDISHI BORA WA MAANDIKO YA MIRADI ILI KUZIWEZESHA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA KUPATA PESA ZA MIRADI YA KIMKAKATI

    March 08, 2024
  • MAANDIKO BORA KUZIWEZESHA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA KUPATIWA MIKOPO KWENYE TAASISI ZA FEDHA

    March 25, 2024
  • LAAC: HATUTAKUBALI SERIKALI IPATE HASARA

    March 21, 2024
  • Angalia Zote

Wasiliana Nasi

Local Government Loans Board

Sanduku la Barua: P.O Box 2710

Simu: +255 26 2321730

Barua Pepe: barua@lglb.go.tz

Fax:

Viungo vya Haraka

  • Watumishi Portal
  • President's Office, Regional Adminstration and Local Government
  • MATUKIO

Zinazohusiana

  • Chuo cha Serikali za Mitaa
  • OR-TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • TAMISEMI BLOG
  • Benki ya Maendeleo (TIB)

Video Mpya

More Videos
    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Sitemap
    • Huduma

Haki Miliki@ Bodi ya Mikoya Mikopo ya Serikali za Mitaa